GOOD NEWS FOR ALL VOLUNTEERS!

Hi, kwa wana Restless Development na vijana wote!

Restless Development Volunteers Udom Club tungependa kuwaomba vijana wote mtumie muda wenu vizuri kuwaelimisha na kuhamasisha watu ili waweze kushiriki vyema kabisa katika harakati hizi za zoezi linaloendelea la sensa la kuhesabu watu na makazi wanamoishi.

Sisi tunaamini zoezi hili ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu pamoja na kuwepo changamoto zinazoikabili ambazo wengi wetu vijana zimeshatukuta au zinaendelea kutupata ambazo kiuhalisia tunabidi tuzitazame upya na kwa umakini wa namna yake ili muafaka uweze kupatikana lakini huu ni wasaa wa kuonyesha mabadiliko ya kweli.Kwa maana hiyo tunaomba sana wadau ushirikiano wenu kwenye hili maana tunaamini,mabadiliko yanaanzia kwako kijana mwenyewe na si vinginevyo.

Wana Restless Development na vijana wote huu ndio wakati wa kuonyesha mabadiliko tukianzia na zoezi hili la Sensa tunaombeni sana ushiriki wenu na uhamasishaji juu ya suala hili.Tunaamini tutapata ushirikiano wenu na mtajitoa kufanya harakati hizi kwa hali zenu zote.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu na amini tupo pamoja wadau wetu na kiujumla wenu tunawatakia heri ya sikukuu ya eid el fitri.
Asanteni,tunawapenda wote.

"Restless Development ya vijana wote, wa rika zote na mahali popote"




No comments: